HISTORIA YA KAMPUNI

Kampuni hii ilianzishwa mwaka 1998 na mkurugenzi mwanzilishi ndugu Philemon Nathan Mtewele, kampuni hii ilianzishwa kwa malengo ya kutoa huduma za pembejeo za kilimo na usafirishaji katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania na Nchi jirani kama, Malawi na Zambia. Baadae ilipanua huduma zake na kuongeza huduma za Bima ikiwa kama wakala wa Zanzibar Insurance.Kwa huduma za kifedha ni wakala wa CRDB(Fahari huduma), NMB na NBC.Pia ni wakala wa TANESCO ambao tunatoa huduma bora ya kuuza LUKU. Tunapatikana Njombe mtaa wa Posta Nyuma ya kanisa la Lutherani kwenye jengo la ghorofa ya Mtewele.Maduka yetu yapo Kituo kikuu cha mabasi Njombe karibu na geti kuu la kutokea magari,Mtaa wa TFA na Mtaa wa Railway barabara iendayo Mabatini Sekondari.Huduma zetu za kifedha,bima na uuzaji wa Luku zinatolewa kwenye jengo la Mtewele lililoko mkabala na Milimani Motel.Pia tunapatikana Mbinga Mtaa wa Mission.

NDOTO ZETU

Ni kuwa kampuni inayoongoza kwa utoaji huduma bora na bidhaa bora kwa wateja wetu nchini Tanzania na kwa kuanzia tumejikita katika mikoa ya nyanda za juu kusini.Kwa hili tuhakikisha kuwa tunamfikia mteja pale alipo moja kwa moja na kupitia mawakala wetu walioko mkoani Njombe na nje ya mkoa. Tunaamini kuwa kwa kutoa huduma bora kampuni yetu itakuwa imejijengea uaminifu kwa wateja wake na hivyo kuwa kampuni bora na kimbilio kwa wakulima na wateja wa huduma nyingine tuzitoazo.

NAMNA TUNAVYO WAFIKIA WATEJA WETU

Kampuni yetu imejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa mteja anafikiwa pale alipo ili kumpunguzia gharama za kuendesha kilimo, huduma hii tunaitoa kupitia mawakala wetu walioko sehemu mbalimbali ikiwemo mikoa ya nyanda za juu kusini kama Uyole katika jiji la Mbeya, Ruvuma, Iringa , na songwe Pia tunawatembelea wakulima ili kubadilishana mawazo juu ya huduma zetu na kilimo kwa ujumla, hili hufanyika hasa kupitia wataalamu wetu wa kilimo wa kampuni. Kampuni yetu inajivunia kuwa na wafanyakazi bora ambao wako makini katika kutoa huduma kwa wateja wetu ili kuwafanya wateja wetu waridhike na huduma zetu, Motto wetu katika utoaji huduma ni "Kwahuduma na bidhaa bora" Na tunajali mda wako mteja.