Latest News

AGRICULTURAL SPRAYER PUMP

Sprayer pump- Ni vifaa maalum vinavyo tumika kunyunyizia viuatilifu(sumu) kwenye mazoa ili kudhibiti visumbufu vya mazoa. Mabomba yametengenezwa kwa kukidhi mahitaji mbalimbali ,mabomba haya yana Nozeli sahihi ambazo zinatoa matone sahihi na yanayo fika kwenye kisumbufu lengwa .

MBEGU

Kampuni yetu mtewele general traders tunauza na kusambaza mbegu za mazao mbalimbali mahindi ,soya,Alizeti,mbegu ya mbogamboga za makapuni mbalimbali. Kwa upande mmbegu za mahindi tuna zinazo komaa kuanzia siku 135-150 mfano PAN 691,SC 719,UH 6303 ,pia tuna za muda mfupi kama SC 403 & 419. Mbegu za mbogamboga-Tunauza na kusambaza mbegu zenye ubora zinazo vumilia magonjwa eg Vitunguu ,kabichi,nyanya ,karoti,Figiri,Hoho n.k.

VIUA KUVU/FUNGICIDES

Viua kuvu:-Ni viuatilifu vinavyo dhibiti kuvu kwenye mazao ,viua kuvu kuna vinavyo zuia/preventive na vinavyo tibu/curative. Vinavyo zuia/preventive-Hivi ni viuatilifu vinavyo fanya kazi ya kuzuia mazao yasishambuliwe na mara nyingi hutumiwa hata kama hujaona dalili za ugonjwa shambani Mfano ; Farmzeb 80 WP(Mancozeb) ,Z-force( Mancozeb),Chloroforce (Chlorothalonil ) ,ebony (Mancozeb) n.k.

VIUA GUGU/HERBICIDES

VIUA GUGU-Ni viuatilifu vinavyo tumika kwenye palizi na kusafisha mashamba. Viuatilifu hivi vimegawanyika kwenye makundi kadhaa Pre –emergence/Vinatumika kabla ya magugu au zao kuota mfano Sure start na Primagram hutumika kuzuia magugu kuota kwenye mahindi na hutumika baada ya kupanda mahindi.

VIUA DUDU /INSECTICIDES

VIUA DUDU/INSECTICIDES-Ni sumu inayotumika kuua,kufukuza wadudu wanao shambulia mazo shambani au gharani.Viua dudu vinajulikana kama Viuatilifu ambavyo vina kiambata amilifu ambacho ndicho kinafanya kazi ya kuua,kufukuza na kuzuia mazao yasishambuliwe na visumbufu,mfano wa visumbufu wadudu,magonjwa na magugu.