Articles

VIUATILIFU NA MBEGU

VIUA KUVU/FUNGICIDES

Viua kuvu:-Ni viuatilifu vinavyo dhibiti kuvu kwenye mazao ,viua kuvu kuna vinavyo zuia/preventive na vinavyo tibu/curative. Vinavyo zuia/preventive-Hivi ni viuatilifu vinavyo fanya kazi ya kuzuia mazao yasishambuliwe na mara nyingi hutumiwa hata kama hujaona dalili za ugonjwa shambani Mfano ; Farmzeb 80 WP(Mancozeb) ,Z-force( Mancozeb),Chloroforce (Chlorothalonil ) ,ebony (Mancozeb) n.k.

VIUATILIFU NA MBEGU

VIUA GUGU/HERBICIDES

VIUA GUGU-Ni viuatilifu vinavyo tumika kwenye palizi na kusafisha mashamba. Viuatilifu hivi vimegawanyika kwenye makundi kadhaa Pre –emergence/Vinatumika kabla ya magugu au zao kuota mfano Sure start na Primagram hutumika kuzuia magugu kuota kwenye mahindi na hutumika baada ya kupanda mahindi.

VIUATILIFU NA MBEGU

VIUA DUDU /INSECTICIDES

VIUA DUDU/INSECTICIDES-Ni sumu inayotumika kuua,kufukuza wadudu wanao shambulia mazo shambani au gharani.Viua dudu vinajulikana kama Viuatilifu ambavyo vina kiambata amilifu ambacho ndicho kinafanya kazi ya kuua,kufukuza na kuzuia mazao yasishambuliwe na visumbufu,mfano wa visumbufu wadudu,magonjwa na magugu.

MBOLEA

MBOLEA ZA KUNYUNYIZIA

Ni mbolea ambazo hutumika kunyunyizia kwenye majani ya mazao husika kwa lengo la kuchochea ukuaji na kuboresha mavuno.Mbolea hizi huchanganywa na maji kwa kiwango ambacho kinakubarika.

MBOLEA

MBOLEA ZA KUKUZIA

Mbolea za kukuzia;Ni mbolea zenye kiwango kizuri cha kirutubisho cha Naitrojeni (N) ambacho kazi yake kubwa ni kuupa mmea ukijani kibichi ili mmea uweze kujitengenezea chakula chake na kuufanya mmea kukamilisha mzungunguko wake wa maisha.Mfano wa mbolea hizi ni :-

MBOLEA

MBOLEA ZA KUPANDIA

Mbolea za kupandia;Ni mbolea zenye kiwango kizuri cha kirutubisho cha Fosforasi (P) ambacho kazi yake kubwa ni kuchochea ukuaji wa mizizi ili iweze kuchukua chakula(virutubisho) na maji kwenye udongo.Mfano wa mbolea hizi ni :-