Kampuni ya Mtewele general traders & Insurance agency wakiwa kwenye maandalizi ya maonyesho ya 08/08 Mbeya tarehe 31/7/2022 yanayoendelea na ambayo yanatarajia kufika kilele tarehe 08/08 ambapo mgeni rasmi atakuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan.
Mtewele General traders ikipokea tunzo ya mshindi wa tatu Tanzania kwenye mauzo ya mbolea za Yara hafla hii ilifanyika 29/7/2022 Dar es salaam. ,Napia Kujiandaa katika msimu wa mwaka 2022/2023
Mtewele General Trades Tukitowa mafunzo kwa wakulima wa parachichi 🥑, Mahindi 🌽, viazi na Mbogamboga🥬🥦 Wilaya ya njombe Kata ya mtwango Kijiji Cha Mawande. Ambapo walipewa elimu juu ya mbolea ipi inafaa kwa mazao hayo kwa nyakati za Kupandia,kukuzia na mbolea ya majani , Pia wali elimishwa Viuatilifu Bora kwa mazao hayo. Mafunzo hayo yaliongozwa na Bwana Musa Lwinga ( Agronomist/Bwana shamba ) wa kampuni .
Kampuni ya mtewele general traders imewafikia wakulima wa zao la parachichi Kijiji Cha makowo tarehe 5/6/2022 na wanandelea kunufaika na pembejeo Bora kutoka kampuni yetu.
Kampuni ya Mtewele General Traders ya Njombe, Tumekabidhi zawadi za kwa washindi wa mashindano ya mpira wa miguu kwa wanaume kombe la Miyao AMCOS yaliyofanyika katika kijiji cha Miyao Wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.
Kampuni ya MTEWELE GENERAL TRADERS ikishirikiana na kampuni ya ROSPER INTERNATIONAL Co. LTD ya Japan imegawa bure taulo za kike kwa wanafunzi wa kike wa shule za sekondari mkoani Njombe. Zoezi hili limefanyika shule ya sekondari Mpechi ambapo zaidi ya shule 18 zimegawiwa taulo hizo kiasi cha katoni zaidi ya 2,600 zenye thamani ya Tsh. 83,000,000/= Milion themanini na tatu.
Matukio katika picha Ni ligi ya MIYAO AMCOS(Mbinga-Ruvuma) iliyodhaminiwa na MTEWELE GENERAL TRADERS Bwanashamba wetu Roden Kulanga akikabidhi jezi za waamuzi na kalenda ya Kampuni Hongereni sana MIYAO kwa ubunifu na tunashukuru kwa kuchagua MTEWELE GENERAL TRADERS katika huduma za pembejeo na ushauri wa kitaalam.
Tukitoa elimu Iliyoambatana na uzinduzi wa duka jipya la wakala wa Mtewele General traders Kijiji Cha Mamongoro.Pamoja za elimu juu ya matmizi sahihi ya mbolea zetu ikiwemo mbolea za kupandia ,mbolea za kukuzia pamoja na mbolea za kubebeshea kwa mazao yote ya nafaka(mahindi,uwele,ngano,mtama,shayiri) na mbogamboga (viazi)
ORODHA YA MADUKA YETU NA MAENEO YALIPO 1. DUKA LETU LIPO MBINGA MJINI BARABARA YA KUELEKEA KANISA LA ROMANI KATOLIKI KARIBU NA BENKI YA NMB. 2.DUKA LETU LIPO MJIMWEMA ENEO LA STENDI MPYA BARABARA YA NJOMBE-SONGEA JENGO LA MASISTA CHUMBA NAMBA MOJA. 3.DUKA LETU LIPO BARABARA YA NJOMBE-SONGEA JIRANI NA KITUO CHA MAFUTA GAPCO. 4.DUKA LETU LIPO BARABARA YA NJOMBE-SONGEA MTAA WA RAILWAY NJIA YA KUELEKEA GROLY HOTEL.
MIONGONI MWA MASHAMBA DARASA MKOANI NJOMBE. Mashamba darasa haya yamefanyika kwa vitemdo kwakutumia mbolea aina ya YARAMILA WINNER kwa zao la viazi mviringo na kuhudumiwa vyema kwa viuatilifu husika .
Upandaji Wa Shamba Darasa La Mahindi Aina Ya Tembo 719 Kuotoka Kampuni Ya Seedco Kijiji Cha Mtwango Wilaya Ya Njombe. Kwa kufuata kanuni bora za upandaji,Nafasi pendekezi ni sentimeta 75 mtari kwa mtari na sentimeta 30 kati ya shimo hadi shimo (Punje moja kwa shimo)
Elimu Kuhusu Matumizi Bora Ya Mbolea Na Viuatilifu Kwenye Zao La Parachihi Kijiji Cha Ulembwe, MKULIMA ALIELIMISHWA YA FUATAYO: Elimu bora juu ya uandaaji wa miche ya parachichi kwenye kitaru,Pia namna bora ya Uandaaji wa Shamba kwaajili ya Zao la parachichi na mbolea shahihi ya kupandia na kukuzia zao la parachichi (Faida za kutumia HAKIKA kwenye zao la parachichi) Pia Namna bora cha kupambana/ kudhibiti magonjwa na wadudu kwenye zao la parachichi. Mafunzo hayo yaliongozwa na Bwana Musa Lwinga ( Agronomist/Bwana shamba ) wa kampuni, Afisa masoko ALEX MAHENGE