FOR ALL INSURANCES AND AGRICULTURE INPUTS
Ili kilimo kilipe,unahitaji pembejeo sahihi.Mbolea ya YaraRega inatoa suluhisho la lishe ambalo linabadilisha mazao yako ya viazi na parachichi kuwa mazao ya kiwango cha soko la kimataifa.Kutoa lishe kamili siyo tu kunalinda mmea,bali kunaongeza uzito,ukubwa,na ubora wa mavuno yako.Wekeza kwenye mbolea bora kwa mavuno bora.Mtewele General Traders tumewaletea YaraRega 13-4-25,ufunguo wako wa kilimo chenye tija.
Tunapoelekea kilele cha Maonyesho ya Wakulima na Wafugaji(Nane Nane) kanda ya Nyanda za juu Kusini,tunawakaribisha wananchi na wadau wote kutembelea banda letu lililopo viwanja vya John Mwakangale,Mbeya .Hii ni fursa ya pekee kwako kujionea na kujifunza kuhusu huduma na bidhaa bora,pamoja na ushauri wa kitaalamu utakaosaidia kupiga hatua zaidi.
Kampuni ya Mtewele General Traders Kwa kushirikiana na CRDB ,CROSE tukiendelea kuhudumia wakulima Wilaya ya wanging'ombe , tunaendelea kuhimiza wakulima kutumia bidhaa Bora kutoka Mtewele General Traders.
Kampuni ya Mtewele General Traders imewafikia wakulima wa Kijiji Cha Ngamanga Halmashauri ya Makambako Waki sogezewa huduma mpaka karibu ,ambapo wamehudumiwa kama kikundi wakielimishwa na wataalamu wetu juu ya matumizi sahihi ya Mbolea,Mbegu za mahindi na Viuatilifu. Tembelea maduka yetu yaliyopo mkoa wa NJOMBE , RUVUMA na MBEYA na maeneo mengine ujipatie Bidhaa bora na Huduma Bora kwa uharaka na kilimo chenye uhakika.
TUNATAMBUA UMUHIMU WA KILA MMOJA WETU TUNAWASHUKURU SANA. NA TUNAWATAKIA BARAKA TELE ZA MWAKA MPYA 2025 TUNAWASHUKURU SANA NA KARIBU TUANZE PAMOJA MWAKA HUU 2025. TUKIMTANGULIZA MUNGU WETU WA MBINGUNI.
Bwanashamba (MUSA LWINGA) Kampuni ya Mtewele General Traders akihojiwa na vyombo vya habari kuhusu namna gani tumejipanga kuhudumia wakulima msimu 2023/2024 na namna gani wakulima wanaweza kuzalisha kwa tija ,kwenye maonyesho ya Yara Expo. Mbeya katika vinjwa vya JOHN MWAKANGALE kuanzia tarehe 24 july 2023 hadi 28 july 2023
Afisa Masoko kutoka kampuni ya Mtewele General Traders (BENEDICTO MGAYA) akimhudumia mteja kwenye maonyesho ya Yara Expo 2023/2024 Mbeya katika vinjwa vya JOHN MWAKANGALE kuanzia tarehe 24 july 2023 hadi 28 july 2023