Mbolea za kukuzia;Ni mbolea zenye kiwango kizuri cha kirutubisho cha Naitrojeni (N) ambacho kazi yake kubwa ni kuupa mmea ukijani kibichi ili mmea uweze kujitengenezea chakula chake na kuufanya mmea kukamilisha mzungunguko wake
wa maisha.Mfano wa mbolea hizi ni :-
i.YaraVera Amidas : Ni mbolea yenye virutubisho viwili 40%N
na 5.6
S ,ni mbolea ya kukuzia zao la mahindi ,mahindi kuanzia majani 5-8 .
ii.Urea Amigran(
46%N): Ni mbolea inayotumika kukuzia mazao mbalimbali
iii.Yarabela Sulfan: Ni mbolea yenye virtutubisho viwili
(primary & secondary nutrients) Naitrojeni na Sulfa inafanya vizuri kwenye mazao ya nafakana mfano mahindi yanapo karibia kuviriga na mbogamboga mfano Viazi,Nyanya nk.
iv.Yaraliva Nitrabor: Mbolea hii ina virutubisho vitatu Naitrojeni,Boron na Calsium (Ca)
,ni mbolea inayo fanya vizuri kwenye mazao mengi kama kukuzia kwenye Nyanya,Viazi,Vitunguu ,karoti na pia inatumika kukuzia zao la parachichi kwenye hatua ya maua na matunda.
v. Yara Mila Winner: Ni NPK yenye
virutubisho
nane
ambayo
inaupa
mmea
klishe
linganifu,mbolea
hii
inatumika
kwenye
kukuzia
matunda
na
mbogamboga
eg
Nyanya,viazi
,parachichi,Vitunguu
nk.
vii.Yarabela CAN
~27N : Ni mbolea ya kukuzia mazoa mbalimbali yenye kirutubisho cha Naitrojeni (N)
,mara nyingi mbolea hizi hutumika kwenye mazao ya nafaka na mbogamboga .
VIII.Sulphate
of Ammonium (SA): ,Ni mbolea yenye virutubisho viwili 21%N
na 24%S
inatumika kukuzia mazoa mengi
IX.Urea
46%N: Ni mbolea inayotumika kukuzia mazao mfano mahindi hii mbolea hutumika mahindi yakiwa na majani 5-8
X.YaraMila
Cereal: Ni NPK 23-10-5+3S+2MgO+0.3Zn ,hii mbolea inatumika kukuzia zao la mahindi,ngano,mtama nk mfano mahindi inawekwa mara tatu ,moja wakati mahindi yakiwa na majani 2 ,pili mahindi yakiwa na majani 5-8 na mara ya tatu mahindi yakiwa yanakaribia kuviriga .
XI.Yaramila Java: Ni NPK 22-6-12 +3S+1MgO+0.2B+0.1Zn inafaa Zaidi kutumika kwenye mazoa jami ya miti mfano Chai na wakati mwingine inaweza kutumika kwenye zao la Parachichi.
XII. NPK
25-5-5 +3S : Mbolea hii inatumika kukuzia mazao mengi ,lakini ni mbolea inayo fanya vizuri kukuzia zao la
chai na mazao mengine aina ya mbogamboga.
NB:Kiwango cha matumizi kwa ekari kitategemea aina ya zao na Afya ya udongo .
KARIBU TUKUHUDUMIE MTEJA
TUNAPATIKANA: NJOMBE,CCM Road / Post Office Behahind Lutheran Church,Plot No.246, Block J, Second Floor
PIGA SIMU: +255 754 268 605 / +255 753 947 715 / +255 754 781 519
Barua Pepe: info@mgt.co.tz
Comments