Upandaji Wa Shamba Darasa La Mahindi Aina Ya Tembo 719 Kuotoka Kampuni Ya Seedco Kijiji Cha Mtwango Wilaya Ya Njombe. Kwa kufuata kanuni bora za upandaji,Nafasi pendekezi ni sentimeta 75 mtari kwa mtari na sentimeta 30 kati ya shimo hadi shimo (Punje moja kwa shimo)
Elimu Kuhusu Matumizi Bora Ya Mbolea Na Viuatilifu Kwenye Zao La Parachihi Kijiji Cha Ulembwe, MKULIMA ALIELIMISHWA YA FUATAYO: Elimu bora juu ya uandaaji wa miche ya parachichi kwenye kitaru,Pia namna bora ya Uandaaji wa Shamba kwaajili ya Zao la parachichi na mbolea shahihi ya kupandia na kukuzia zao la parachichi (Faida za kutumia HAKIKA kwenye zao la parachichi) Pia Namna bora cha kupambana/ kudhibiti magonjwa na wadudu kwenye zao la parachichi. Mafunzo hayo yaliongozwa na Bwana Musa Lwinga ( Agronomist/Bwana shamba ) wa kampuni, Afisa masoko ALEX MAHENGE
Mafunzo Juu Ya Matumizi Sahihi Ya Mbolea Ya Kiasili Ya Hakika na Viuatilifu Bora Kwenye Zao La Parachichi Katika Kijiji Cha Usita Kata Ya Ulembwe. Mafunzo hayo yaliongozwa na Bwana Musa Lwinga ( Agronomist/Bwana shamba ) wa kampuni .
Wakulima wakipewa elimu namna bora ya kupanda wa Viazi kwa vitendo kwa kuzingatia umbali kati ya kiazi kimoja na kingine pia umbali kati ya mtari mmoja wa viazi na mwingine na mbolea gani ni nzuri kwa viazi ,Viuatilifu gani na muda gani unapaswa kukuzia ikiwa mmea una hali gani, Yote hayo yalifanyka kijiji cha Lugenge Halmashauri ya Mji Njombe.
Wakulima wakifundishwa matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo kutoka kampuni Mtewele General traders , Mkoani NJOMBE juu ya Mbinu za masoko na wakulima kubadilika Kuoka kilimo cha asili kwenda kwenye kilimo chenye tija (kisasa) , Pia Kuzijua aina za mbolea na matumizi yake ,hapa ni kijiji cha KIYAULA kata ya LUGENGE. Mafunzo hayo yalikiongozwa na Bwana Musa Lwinga ( Agronomist/Bwana shamba ) wa kampuni