Latest News

KAMPUNI YA MTEWELE GENERAL TRADERS ,IKITOA MAFUNZO YA KILIMO CHA PARACHICHI NA NAMNA BORA YA MATUMIZI YA MBOLEA NA VIUATILIFU.

Kampuni ya Mtewele General Traders ,umetoa mafunzo ya kilimo Cha Parachichi na namna Bora ya matumizi ya mbolea na viuatilifu kudhibiti wadudu na Magonjwa ,mafunzo haya yametlewa katika Kijiji Cha Itipingi ,Halmashauri ya Njombe vijijini Tarehe 23/5/2023

MAFUNZO YA NAMNA BORA YA KUZALISHA ZAO LA PARACHICHI KIJIJI CHA LUPEMBE WILAYA YA NJOMBE VIJIJINI

Afisa masoko ,kampuni ya Mtewele general traders akitoa namna gani mkulima ananufaika na bidhaa zetu ,wakati wa mafunzo ya namna Bora ya kuzalisha zao la parachichi Kijiji Cha Lupembe wilaya ya Njombe vijijini tarehe 27/5/2023

ELIMU YA MATUMIZI SAHIHI YA MBEGU NA MBOLEA PAMOJA NA MBINU ZINGINE ZA UZALISHAJI WA MAHINDI KIJIJI CHA DULAMU

Kampuni ya Mtewele General traders kwa kushirikiana na wadau wake OCP Tanzania na Bayer wakitoa elimu ya matumizi sahihi ya mbegu na mbolea pamoja na mbinu zingine za uzalishaji wa mahindi Kijiji Cha Dulamu ,Halmashauri ya Wanging'ombe tarehe 26/5/2023

WAKULIMA KIKUNDI CHA MUUNGANO KIJIJI CHA MTILA

Wakulima kikundi Cha Muungano Kijiji Cha Mtila , kata Matora ,Halmashauri ya Njombe mji mkoa wa Njombe ,wakishiriki mafunzo ya kilimo Bora Cha Parachichi ,Viazi na Ngano kutoka kampuni ya Mtewele General traders tarehe 27/5/2023.

MTEWELE GENERAL TRADERS TUKIENDELEA KUGAWA MBOLEA YA RUZUKU KWA WAKULIMA

Wakulima Wa Kijiji Cha Kitulila,Lusitu,Makowo,Ngalanga,Mlangali,Ludewa Wakiendelea Kupata Mbolea Za Ruzuku Kupitia Mtewele Geneeral Traders Ambapo Tunaendelea Kusambaza Vijijini Katika Mkoa Wa Njombe Na Wilaya Zake Zote ,Pia Tunatarajia Kosogeza Huduma Ya Kugawa Mbolea Katika Maeneo Mengine Ikiwemo Ruvuma,Iringa ,Mbeya Tukizingatia Taratibu Na Miongozo Toka Mamlaka Ya Udhibiti Wa Mbolea Kitaifa (Tfra)

MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE - NANENAE 2022

Kampuni ya mtewele general traders walitembelewa na M/kiti Halmashauri ya Mji Njombe tarehe 1/8/2022 kwenye maonyesho ya 88 yanayoendelea na ambayo yanatarajia kufika kilele tarehe 08/08 ambapo mgeni rasmi atakuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan.

NANE NANE 2022

Kampuni ya Mtewele general traders & Insurance agency wakiwa kwenye maandalizi ya maonyesho ya 08/08 Mbeya tarehe 31/7/2022 yanayoendelea na ambayo yanatarajia kufika kilele tarehe 08/08 ambapo mgeni rasmi atakuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan.