Latest News

Kugawa Bure Taulo Za Kike Kwa Wanafunzi Wa Kike Wa Shule Za Sekondari Mkoani Njombe ( Tarehe 13/05/2022)

Kampuni ya MTEWELE GENERAL TRADERS ikishirikiana na kampuni ya ROSPER INTERNATIONAL Co. LTD ya Japan imegawa bure taulo za kike kwa wanafunzi wa kike wa shule za sekondari mkoani Njombe. Zoezi hili limefanyika shule ya sekondari Mpechi ambapo zaidi ya shule 18 zimegawiwa taulo hizo kiasi cha katoni zaidi ya 2,600 zenye thamani ya Tsh. 83,000,000/= Milion themanini na tatu.

LIGI YA MIYAO AMCOS(MBINGA-RUVUMA) ILIYODHAMINIWA NA MTEWELE GENERAL TRADERS

Matukio katika picha Ni ligi ya MIYAO AMCOS(Mbinga-Ruvuma) iliyodhaminiwa na MTEWELE GENERAL TRADERS Bwanashamba wetu Roden Kulanga akikabidhi jezi za waamuzi na kalenda ya Kampuni Hongereni sana MIYAO kwa ubunifu na tunashukuru kwa kuchagua MTEWELE GENERAL TRADERS katika huduma za pembejeo na ushauri wa kitaalam.

UZINDUZI WA DUKA JIPYA LA WAKALA WA MTEWELE GENERAL TRADERS KIJIJI CHA MAMONGORO

Tukitoa elimu Iliyoambatana na uzinduzi wa duka jipya la wakala wa Mtewele General traders Kijiji Cha Mamongoro.Pamoja za elimu juu ya matmizi sahihi ya mbolea zetu ikiwemo mbolea za kupandia ,mbolea za kukuzia pamoja na mbolea za kubebeshea kwa mazao yote ya nafaka(mahindi,uwele,ngano,mtama,shayiri) na mbogamboga (viazi)

MIONGONI MWA MASHAMBA DARASA MKOANI NJOMBE

MIONGONI MWA MASHAMBA DARASA MKOANI NJOMBE. Mashamba darasa haya yamefanyika kwa vitemdo kwakutumia mbolea aina ya YARAMILA WINNER kwa zao la viazi mviringo na kuhudumiwa vyema kwa viuatilifu husika .

UPANDAJI WA SHAMBA DARASA LA MAHINDI AINA YA TEMBO 719 KUTOKA KAMPUNI YA SEEDCO KIJIJI CHA MTWANGO WILAYA YA NJOMBE.

Upandaji Wa Shamba Darasa La Mahindi Aina Ya Tembo 719 Kuotoka Kampuni Ya Seedco Kijiji Cha Mtwango Wilaya Ya Njombe. Kwa kufuata kanuni bora za upandaji,Nafasi pendekezi ni sentimeta 75 mtari kwa mtari na sentimeta 30 kati ya shimo hadi shimo (Punje moja kwa shimo)

ELIMU KUHUSU MATUMIZI BORA YA MBOLEA NA VIUATILIFU KWENYE ZAO LA PARACHIHI KIJIJI CHA ULEMBWE

Elimu Kuhusu Matumizi Bora Ya Mbolea Na Viuatilifu Kwenye Zao La Parachihi Kijiji Cha Ulembwe, MKULIMA ALIELIMISHWA YA FUATAYO: Elimu bora juu ya uandaaji wa miche ya parachichi kwenye kitaru,Pia namna bora ya Uandaaji wa Shamba kwaajili ya Zao la parachichi na mbolea shahihi ya kupandia na kukuzia zao la parachichi (Faida za kutumia HAKIKA kwenye zao la parachichi) Pia Namna bora cha kupambana/ kudhibiti magonjwa na wadudu kwenye zao la parachichi. Mafunzo hayo yaliongozwa na Bwana Musa Lwinga ( Agronomist/Bwana shamba ) wa kampuni, Afisa masoko ALEX MAHENGE

MAFUNZO JUU YA MATUMIZI SAHIHI YA MBOLEA YA KIASILI YA HAKIKA NA VIUATILIFU BORA KWENYE ZAO LA PARACHICHI KATIKA KIJIJI CHA USITA KATA YA ULEMBWE

Mafunzo Juu Ya Matumizi Sahihi Ya Mbolea Ya Kiasili Ya Hakika na Viuatilifu Bora Kwenye Zao La Parachichi Katika Kijiji Cha Usita Kata Ya Ulembwe. Mafunzo hayo yaliongozwa na Bwana Musa Lwinga ( Agronomist/Bwana shamba ) wa kampuni .