Latest News

MTEWELE GENERAL TRADERS TUKIENDELEA KUGAWA MBOLEA YA RUZUKU KWA WAKULIMA

Wakulima Wa Kijiji Cha Kitulila,Lusitu,Makowo,Ngalanga,Mlangali,Ludewa Wakiendelea Kupata Mbolea Za Ruzuku Kupitia Mtewele Geneeral Traders Ambapo Tunaendelea Kusambaza Vijijini Katika Mkoa Wa Njombe Na Wilaya Zake Zote ,Pia Tunatarajia Kosogeza Huduma Ya Kugawa Mbolea Katika Maeneo Mengine Ikiwemo Ruvuma,Iringa ,Mbeya Tukizingatia Taratibu Na Miongozo Toka Mamlaka Ya Udhibiti Wa Mbolea Kitaifa (Tfra)

MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE - NANENAE 2022

Kampuni ya mtewele general traders walitembelewa na M/kiti Halmashauri ya Mji Njombe tarehe 1/8/2022 kwenye maonyesho ya 88 yanayoendelea na ambayo yanatarajia kufika kilele tarehe 08/08 ambapo mgeni rasmi atakuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan.

NANE NANE 2022

Kampuni ya Mtewele general traders & Insurance agency wakiwa kwenye maandalizi ya maonyesho ya 08/08 Mbeya tarehe 31/7/2022 yanayoendelea na ambayo yanatarajia kufika kilele tarehe 08/08 ambapo mgeni rasmi atakuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan.

Mtewele General Traders Akiwa Moja Ya Mawakala Wakubwa Wa Yara Tanzania Anashiriki

Mtewele General traders ikipokea tunzo ya mshindi wa tatu Tanzania kwenye mauzo ya mbolea za Yara hafla hii ilifanyika 29/7/2022 Dar es salaam. ,Napia Kujiandaa katika msimu wa mwaka 2022/2023

MAFUNZO KWA WAKULIMA WA PARACHICHI,MAHINDI,VIAZI NA MBOGAMBOGA - MKOANI NJOMBE

Mtewele General Trades Tukitowa mafunzo kwa wakulima wa parachichi 🥑, Mahindi 🌽, viazi na Mbogamboga🥬🥦 Wilaya ya njombe Kata ya mtwango Kijiji Cha Mawande. Ambapo walipewa elimu juu ya mbolea ipi inafaa kwa mazao hayo kwa nyakati za Kupandia,kukuzia na mbolea ya majani , Pia wali elimishwa Viuatilifu Bora kwa mazao hayo. Mafunzo hayo yaliongozwa na Bwana Musa Lwinga ( Agronomist/Bwana shamba ) wa kampuni .

ELIMU KUHUSU UZALISHAJI WA ZAO AINA YA PARACHICHI

Kampuni ya mtewele general traders imewafikia wakulima wa zao la parachichi Kijiji Cha makowo tarehe 5/6/2022 na wanandelea kunufaika na pembejeo Bora kutoka kampuni yetu.

WASHINDI WA MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU KWA WANAUME KOMBE LA MIYAO AMCOS YALIYOFANYIKA KATIKA KIJIJI CHA MIYAO WILAYANI MBINGA MKOANI RUVUMA

Kampuni ya Mtewele General Traders ya Njombe, Tumekabidhi zawadi za kwa washindi wa mashindano ya mpira wa miguu kwa wanaume kombe la Miyao AMCOS yaliyofanyika katika kijiji cha Miyao Wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.