MATUKIO

WASHINDI WA MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU KWA WANAUME KOMBE LA MIYAO AMCOS YALIYOFANYIKA KATIKA KIJIJI CHA MIYAO WILAYANI MBINGA MKOANI RUVUMA

Kampuni ya Mtewele General Traders ya Njombe, Tumekabidhi zawadi za kwa washindi wa mashindano ya mpira wa miguu kwa wanaume kombe la Miyao AMCOS yaliyofanyika katika kijiji cha Miyao Wilayani Mbinga mkoani Ruvuma. Timu ya Kata ya Nyoni iliibuka mshindi wa mashindano hayo na kubeba kombe pamoja na zawadi ya pesa tasilimu. Pamoja na kutoa zawadi kwa washindi wa mpira wa miguu, kampuni ya Mtewele General Traders ilitoa msaada wa katoni 13 za taulo za kike kwa wanafunzi wasichana wa shule ya sekondari Mahilo iliyopo kijijini hapo. Haya yote yanafanywa na kampuni ya Mtewele General Traders katika dhana ya kurudisha faida kwa jamii kutokana na biashara inazofanya ikiwemo uuzaji wa pembejeo za kilimo. Kampuni ya Mtewele General Traders yenye makao yake makuu mkoani Njombe, ina tawi pia katika wilaya ya Mbinga mkoni Ruvuma.

Yefta Msemwa

jepthahcamis@gmail.com

softwaredeveloper, interprenuwers.

Follow Me:

Comments